Zari Aeleza Chanzo Cha Kifo Cha Mama Yake

Mama Mzazi wa Zari ambae ni Mama watoto wa mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz amezikwa jana nyumbani kwao Uganda.

Familia yake ilipata nafasi ya kuzungumzia historia yake kwa ufupi na chanzo cha kifo chake na kusema alifariki kutokana na ugonjwa wa kisukari na uvimbe na kwamba milioni 55 za Uganda ( zaidi ya milioni 34 za Tanzania) ndio zilitumika kumtibu Hospitali ambapo kati ya hizo Zari mwenyewe alichangia milioni 12 za Uganda (zaidi ya milioni 7 za Tanzania).

Halima Hassan alifariki July 20 2017 baada ya kulazwa kwenye Hospitali mbili Uganda ambapo msibani hapo Familia yao imemshukuru sana Shangazi yao ambae alipigana sana kuhakikisha Mama anatibiwa.

Mmoja wa watoto kwenye familia alieleza msibani kwamba Mama yao alipokua akitibiwa South Africa aliwaambia hatopenda kurudi Uganda akiwa kwenye jeneza, ni kama alijua siku zake zimeisha ndio maana alitaka kurudi nyumbani akiwa hai.

Source: Millard ayo