Qboy Msafi asimulia upekee na faida aliyopata Wasafi

Msanii na hitmaker wa ngoma ‘Karorero’ QBoy Msafi amezungumzia kikubwa alichopata katika ushirikiano wa kufanya kazi na Diamond Platnumz na Wasafi kwa ujumla kama msanii pia outfit desgner.

Akizungumzia kuwa nje ya Wasafi na maisha yake kama msanii Qboy amesema kuwa ni mengi yamefanyika na kwa kipindi chote cha ufanyaji kazi na amefaidia kwa kiasi kikubwa tofauti na inavyotazamiwa.

“yaani mimi nina imani kwamba nilipokuwa Wasafi nilikuwa napikika mle ndani yaani kwasababu nimepata experience kubwa sana na naweza kusema nimepata msaada mkubwa sana kutoka kwao na mpaka sasa” Amesema QBoy kupitia ya Tbc Fm.

Hata hivyo QBoy amewashukuru mashabiki kwa support na wasanii ambayo wamempatia kwa kipindi ambacho ameachia wimbo wake mpya mbali na kuwa nje ya ‘WCB Wasafi’.

Source: Dizzimonline