Mr Blue adai anaileta Micharazo ikiwa na wasanii wapya

Msanii mwenye aka nyingi lakini jina kubwa lililokubalika na mashabiki zake, Mr Blue ambaye pia bado anafanya poa na ngoma yake, Mboga Saba aliyomshirikisha Alikiba, amezungumzia suala la kuwasimamia wasanii wachanga ambao wanatamani na wao kufika mbali zaidi kimuziki

Akizungumza na Dizzim Online, Blue amesema ana mawazo hayo tena kwa muda mrefu akisisitiz kuwa pengine yeye ndio alikuwa wa kwanza kufikiria hilo.

“Kiukweli hata mimi nina mawazo hayo, tena mawazo yangu ni ya muda mrefu kwa sababu ukiangalia tulishawahi kutengeneza kundi mimi na Nyandu Tozi kwa ajili ya kusaidia vijana wanaopenda rap, tukaliita Bob Micharazo. Lakini mi bado nina ndoto nyingine kuwepo na Micharazo nyingine ya kwangu mimi kama mimi ambayo watu wengine watakuwepo na nataka nifanya official. Mwanzo ilikuwa kishikaji yaani kiselasela tu,” amesema Blue.

Lakini pia rapper huyo hakuacha kuwaomba mashabiki zake wakae mkao wa kula muda si mrefu ataachia mzigo mpya ingawa hajasema lini hasa na amefanyia wapi.

Source: Dizzimonline

 

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors
muzikizaidi
Author: muzikizaidi