‘Watanzania ninafahamu mna uhuru wa kuzungumza, nawaomba tujielekeze kwenye vitu vya maendeleo, tunajielekeza zaidi kwenye udaku.Nawaomba watanzania kampeni zimeshakwisha ulie lakini Rais ni Magufuli, mimi kwangu ni hapa kazi tu, maendeleo.Mimi ndiye ninayeamua nani atakuwa wapi, kwa hiyo Makonda chapa kazi.Kwa sasa tuko kwenye mchakato wa kujenga barabara kutoka DSM kwenda Chalinze kwa barabara ya njia Sita.Tupo hapa kusaini mkataba wa mkopo na kuweka jiwe la msingi, namshukuru sana Rais wa benki ya dunia.
Source: millard ayo