Diamond amtambulisha msanii mpya WCB,

May 22, 2017 Mwimbaji kutoka WCB ambaye anafanya vizuri kwenye Bongofleva Diamond Platnumz kupitia Clouds 360 ya Clouds TV amemtambulisha msanii mpya ambaye atakuwa mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo.

Katika utambulisho huo Diamond amesisitiza kuwa anawajibika kuwasaidia wengine kwa kuwa hata yeye amesaidiwa ndiyo maana amefikia hatua hiyo hivyo anapenda na wengine wakifikia mafanikio kama yake kwa kuwasaidia.

“Ujio wangu hapa leo ni kwa ajili ya kumtambulisha kijana wetu mwingine kama sehemu ya kuwasaidia wengine. Nawashukuru sana Clouds Media kuwa kama daraja kuwasaidia wengine. Kama nisingesaidiwa nisingefika hapa. Inapotokea mtu anasaidiwa nashiriki kwa kidogo nilichonacho kwa sababu mimi nisingesaidiwa nisingefika hapa.

“Kama mimi nilisaidiwa ni nafasi yangu kuwaunga mkono kuwasaidia wengine walio katika matatizo. Nakumbuka Kipepeo nilitoa Tsh. 5m. Huu ni msimu wa shukrani mimi namshukuru kila mtu na nawashukuru sana Clouds FM kwa sababu wamenisaidia.

“Moto wa Clouds ni Redio Ya Watu, na Televisheni Ya Watu kwa hiyo nawashukuru kwa sababu hawaishii kwenye burudani tu wanakuwa karibu na watu kwa kuishi kwenye maisha yao halisi. Nafahamu mangapi Clouds wamenisaidia na siwezi kusahau.” – Diamond Platnumz.

Source: Millard ayo