Nimenusurika kuuawa Asema Bob Junior.

Msanii na mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Bob Junior ameiambia Dizzim Online kuwa usiku wa kuamkia jana alitolewa na kutishiwa kwa bastola na watu wasiojulikana.

Amesema, ” Usiku wa saa nne maeneo ya Kinondoni Mwanamboka nilikuwa natokea maeneo ya Kinondoni napita Mwana mboka sheli kutia mafuta, so nilivyofika pale pale sheli kuna mambo fulani yalitokea,” amesema muimbaji huyo.

“Ndo wakatokea vijana wa kiarabu wawili wakanitolea bastola kwa bahati nzuri ni bado ilikuwa mapema na mimi nilikuwa na watu kwenye gari so nikanusurika,” ameongeza.

Amesema baada ya tukio hilo alilazimika kuripoti polisi ambao wanafanya uchunguzi. Hadi sasa hajaweza kujua nini lilikuwa lengo la watu hao.

Source: Dizzim Online.

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!