Basi la timu ya Ruvu Shooting limepata ajali


Timu ya Ruvu Shooting  May 21 2017 wakiwa njiani kutokea Shinyanga walipocheza mchezo wao wa kumalizia msimu wa 2016/2017 wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Stand United wamepata ajali wakiwa njiani kurejea Pwani.

Ruvu Shooting wamepata ajali wakiwa maeneo ya Singida kurejea Pwani baada ya bus la timu yao walilokuwa wanasafiria kupasuka tairi ya mbele na kuacha njia, millardayo.com imeongea na kaimu kamanda wa Polisi Singida Isaya Mbugi na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo.


“Ni eneo baada ya kupita eneo la Manyoni mteremko wa kwanza ndio ajali imetokea baada ya tairi ya mbele kushoto ya basi lao kupasuka basi likaacha njia na kwenda pembeni halikuanguka hakuna madhara kwa mchezaji au mtu yoyote“  –

Source: Millard ayo