Matukio Makubwa Yanayomhusu Wema Sepetu.

Wema Sepetu ni mrembo na Staa wa filamu kutoka Tanzania ambaye haishi kupamba vichwa vya habari kila linapoibuka lolote ambalo umhusu huku zaidi akiandikwa kila zinapoibuka dalili za kuwa katika mahusiano na yeyote kwakuwa alishaingia katika mahaba mapaka kuvishwa pete ya uchumba na Staa Diamond Platnumz na wengine kama vile Idris Sultan na TID.

Enzi za Mahaba ya Wema na Diamond Platnumz

Mwaka huu Wema Sepetu alijikuta katika skendo kubwa ya kuonekana kuwa anatoka kimapenzi na Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mhe Freeman Mbowe baada ya kusambaa kwa sauti ambayo kila aliyepata nasafi ya kusikiliza alipeleka mawazo yake moja kwa moja kuwa mazungumzo yale ni ya wawili hao jambo ambalo baadae Mhe Freeman Mbowe alikanusha hilo na kuhisiwa kuwa sauti za mazungumzo yale zilikuwa ni magizo tu ya watu wasiojulikana wenye lengo la kuchafua majina yao.
Mwaka 2012 mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva hasa upande wa Rap/Hip Hop walipokea video ya wimbo ‘”Miss Tanzania” wa msanii wa muziki wa rap Msafiri Kondoo a.k.a Solo Thang na wimbo huu uliwashinda wengi wao kuutafsiri kwakuwa wapo waliodhani Solo Thang alikuwa akiimba kuhusu taifa la Tanzania na wengine wakidhani kuwa aliimba zaidi kuhusu Wema Sepetu kwa kufananisha uandishi na baadhi ya tabia kwakuwa mbali na kuwa ilitumika Bendera ya Tanzania katika video lakini pia litumika mrembo aliyedhaniwa kuwa anatumika kutafsiri tabiza za kilichokuwa kinazungumziwa.

3. Mwaka 2014 Wema Sepetu alifanya tukio la aina yake baada ya kuchukua uamuzi wa kuvamia kituo cha machapisho ya habari cha Global Publishers kwa madai ya kuwa zimeandikwa habari zisizo za kweli kuhusu yeye na aliyekuwa mpenzi wake kwa kipindi hicho Diamond Platnumz kwa kuandikwa taarifa za kuwa anajihuusisha na mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja(Usagaji) kitu ambacho kilimsukuma mpaka kuzivamia ofisi za kituo hicho akimtafuta mhusika wa uandishi wa habari hizo kwa hali shari zaidi tukio ambalo lilisimamisha utaratibu wa kazi kwa muda.

Wema Sepetu

Katika kuyakumbuka haya Wema Sepetu leo kwake kikubwa ambacho anakikumbuka ni mfanano wa siku ya kuzaliwa kwake na anatimiza umri wa miaka 28 ambapo katika umri huu ndani ya umaarufu wake katika tasnia ya filamu anatajwa kuendelea kufanya vizuri kupitia filamu yake mpya ya ‘Heaven Sent’ ambayo ameshirikiana na staa wa filamu wa kiume Salim Ahmed (Gabo).

Wema Sepetu na Gabo

Mbali na watu wake wa karibu kuonekana kumtakia mafanikio mema katika hii siku yake, kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu amewakumbusha mashabiki wa kazi yake ya sanaa na wote wanaopenda anachokifanya hasa waliofuata katika akaunti ya mtandao wa picha wa Instagram kuwa leo ndi siku yake ya kuzaliwa kwa kuandika “And then the queen was born” maneno yalioambatana kwenye picha ambayo aliipiga mgongo na mgongo huo ulionekana kupambwa kwa michoro ya tatoo za maua.

Source: Dizzim Online.