Mbwana Samatta kampokea Himid Mao Ubelgiji

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta usiku wa May 10 ametumia ukurasa wake wa instagram kupost picha ya pamoja na mtanzania mwenzake Himid Mao anayeicheza Azam FC wakiwa wote Ubelgiji

Himid ambaye hivi karibuni alikuwa katika majaribio Denmark katika club ya Randers FC ameonekana ameamua pia kwenda kumtembelea Mbwana Samatta Ubelgiji kutokana na Denmark na Ubelgiji kuwa sio mbali sana, Samatta amepost picha akiwa uwanja wa ndege wa Brussels Ubelgiji na kuandika “Nikiwa na mgeni wangu👍🇹🇿@himid23mao“

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Himid Mao aliondoka Tanzania wiki iliyopita na kwenda Denmark kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika timu ya Randers FC inayoshirikiki Ligi Kuu Denmark na Jumanne hii iliripotiwa kuwa alicheza game ya kirafiki kama sehemu ya majaribio yake.

Source: Millard ayo