Kiungo wa kati wa Uingereza Dele Alli amepigwa marufuku

Kiungo wa kati wa Uingereza Dele Alli amepigwa marufuku kutoshiriki mechi moja ya kimataifa kufuatia hatua yake ya kuinua kidole cha kati wakati wa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Slovenia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 atashiriki mechi dhidi ya Lithuania siku ya Jumapili.

Alli alisema kuwa ishara hiyo ilimlenga aliyekuwa mchezaji mwenza wa Spurs Kyle Walker wakati wa dakika ya 77 ya udhindi wa 2-1 katika kundi F.

Kisa hicho kilitokea baada ya Alli kupigwa kumbo na beki wa Slovakia Martin Skrtel huku refa Clement Turpin akionyesha ishara ya mchezo uendelee.

Ilionekana kana kwamba Alli alimuonyesha ishara hiyo ya kidole cha kati afisa huyo ambaye pia walirushiana maneno alipotolewa nje dakika ya 93.

story@moodyhamza