Mjukuu auwawa kwa kuchapwa viboko na Bibi

Licha ya vitendo vya ukatili kupigwa vita, bado vitendo hivyo vimeendelea kujitokeza baada ya mkazi wa Kijiji cha Mhungwe, Kata ya Mabuki wilayani Misungwi mkoani hapa, kutuhumiwa kumuua mjukuu wake mwenye umri wa miaka saba kwa kumchapa fimbo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema tukio hilo lilitokea Mei 10, saa moja jioni baada ya bibi  kumchapa viboko mjukuu wake akimtuhumu kuchelewa kurudi nyumbani alipoenda kucheza nyumba jirani.

Msangi amesema mtoto huyo Balangi Mika aliporejea nyumbani bibi yake alimkamata na kumchapa fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake na kusababisha kifo chake.

Amesema bibi huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na utakapokamilika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu mashtaka.

 Source: Udaku