PERFUME za Diamond Platnumz Zamzindua ALI Kiba Usingizini…..


Msanii wa muziki Alikiba ametangaza ujio wa bidhaa mbalimbali kutoka katika brand yake ‘AK’ pamoja na ‘King Kiba’.

Muimbaji huyo wa Aje, amesema kuwa hiyo ni mipango mizito na hatarajii kuifanya kiholela kwani hata mwanzo alitoa baadhi ya bidhaa kama promotion.

“AK ni  brand ya Alikiba nashukuru imekuwa kubwa watu wanavaa lakini pia ipo na ya King Kiba nayo ni brand yangu na zipo official kabisa na kazi zitakapoanza watapata product zote,” Alikiba alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Aliongeza,

“Kuna malengo makubwa sana tumeyaweka lakini siwezi kusema sasa hivi ila kuna jeans, viatu na glasses tayari zishatoka soon wataziona maana hizi zitakuwa za kwanza sababu tayari zishatoka na kuna energy drink”

Wiki mbili zilizopita muimbaji mwingine Diamond Platnumz alizindua perfume yake iitwayo, Chibu Perfume.

Source: Millard ayo