Mwimbaji star wa Bongofleva Mo Music kudaiwa kupigana na mdogo wake Mr T touch akiwa Studio baada ya kuwatoa watu nje wakati anarekodi.
Baada ya kuenea taarifa hizo kwenye social media ambapo Mo Music alidaiwa kupigwa na ushindwa kuondoka hadi alipoomba msaada kwa watu wake wa karibu, Soudy Brown alimtafuta na kupiga naye story ili kujua ukweli wa taarifa hizo.Ishu ilikuwa narekodi na nilipofika nikasikia wanaambiwa watoke nje badala ya kutoka nje nikasikia anasema Mo Music kitu gani naye atoke nje. Nilipotoka nje nikaona mtu kanivuta na mimi siyo mnyonge kiasi hicho, nina uwezo wa kupambana pia japo nilitumia hekima haya mambo yaishe.” – Mo Music.
Source: Millard ayo