Nimeondoka Rockstar sio sababu Alikiba

Kama utakumbuka mwaka 2016 mwimbaji Baraka Da Prince alisaini mkataba wa kufanya kazi na label ya Rockstar 4000 lakini baadae zikaanza kusambaa taarifa ambazo zilidai kuwa staa huyo ameachana na label hiyo.

Baraka the Prince amethibitisha kuwa hayupo tena chini ya Rockstar4000 na kuwa anafanya kazi zake binafsi akidai kuna mambo hayapo sawa kati yake na Management huku akisisitiza siyo kwa sababu Alikiba amekuwa Wakurugenzi wa label hiyo.

Kuna vitu lazima uvihoji na ukiona watu unaofanya nao kazi kama kampuni wanakuwa hawajali kitu unachotaka kufahamu kuhusu makubaliano yenu ya kazi inakuwa na mashaka kidogo”

“Naweza kusema sipo chini ya Rockstar kwa sababu mimi ndio boss wa muziki wangu halafu mimi ndio nafanya kazi, kukiwa na vitu haviko sawa kwa upande wangu mimi ndio naweza kutoa kauli ya mwisho, sipo chini ya Rockstaar”

“Kuna vitu haviko sawa hilo neno boss zito sana, unaponiambia mtu ni boss wangu, how? Boss kivipi kwangu? Alikiba kuwa director wa Rockstar mimi ndio nijitoe, hapana…. kuna vitu haviko sawa na uongozi wa Rockstar”

“Nilipokwenda Rockstar4000 sikusaini chini ya AliKiba, mimi nina matatizo binafsi na uongozi na kama mambo hayapo sawa ukiona kitu jua kipo chini ya Baraka” – Baraka the Prince.

Source: Millard ayo