MREMBO Aliyeuawa na EX Wake Kwa Kuchomwa Moto Afrika Kusini


Karabo Mokoena, binti wa Afrika Kusini ambaye takribani wiki mbili zilizopita, habari zake zilienea mitandaoni kuwa anatafutwa kutokana na kupotea kwake tangu April 28, amekutwa amefariki dunia.

Kwa mujibu wa baba yake Karabo, Tshepo Mokoena kupitia mtandao wa Facebook ameripoti kuwa mwanaye amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umechomwa moto. Habari zinasema kwamba, aliyekuwa mpenzi wa mrembo huyo ndiye anayetuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

“The boyfriend has confesses, He killed and burned my daughter,” ameandika Tshepo kwenye mtandao huo. Hata hivyo muuaji wa tukio hilo bado anasakwa na polisi.

Mapema wiki hii rafiki wa karibu wa marehemu, Stephy Leong kupitia mtandao wa Instagram atoa taarifa za kupotea kwa rafiki yake huyo kwa kuandika, “If anyone has seen my friend Karabo from around April 28th, please let me know. She’s been missing since, it’s urgent

Source: Udaku