Shamsa Ford Awachana Wanaume

 


Msanii wa Filamu nchini, Shamsa Ford amewatolea uvivu wanaume wanaopenda kulelewa na wanawake.

Kupitia mtandao wa Instagram muigizaji huyo ameonyeshwa kukerwa na tabia hiyo ambayo inapelekea wawe tegemezi kwa wapenzi hao kutokana na kuchagua kazi.

“Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauri mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii, usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini wakati elimu yako ni darasa la pili. Mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha, sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie riziki.,” ameandika mrembo huyo.

Akaongeza “Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi ukishajiona una sura nzuri basi na wewe eti unadanga kwa jimama lenye pesa. Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa, hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?mara vibenten,vipanyabuku,vichura,vitom and jerry… daaahh

Source: Udaku