Manchester United mchongo mrefu mapato ya £581m

Klabu ya Manchester United imeripoti mapato ya £581m kwa kipindi cha fedha cha 2017 huku mapato ya runinga yakiongezeka.

Katika mwaka mmoja baada ya kushinda kombe la bara Yuropa, na EFL klabu hiyo imetia saini kandarasi 12 za ufadhili huku mapato ya matangazo pamoja na yale yanaopatikana wakati wa mechi yakiongezeka.

Klabu hiyo ilifaidika kutoka kwa ongezeko la mapato ya runinga wakati wa kipindi cha 2016-17 ikiwa ndio mwaka wa kwanza kati ya mitatu ya makubaliano ya matangazo ya runinga.

Klabu hiyo ya Old Trafford ni ya pili katika ligi ya premia.Ina alama sawa na mabao na viongozi wa ligi Manchester City.

Mnamo mwezi Juni tarehe 30 mapato ya matangazo yaliongezeka hadi £194m kutoka £140m mwaka mmoja kabla ikiwa ni ongezeko la silimia 38.

Msimu huu klabu hiyo imerudi katika ligi ya vilabu bingwa baada ya kushinda kombe la Yuropa dhidi ya Ajax mnamo mwezi Mei.

story@moodyhamza