Diego Costa ameondoka Chelsea

soka wa kimataifa wa Hispania mwenye asili ya Brazil Diego Costa usiku wa September 26 2017 amefanikiwa kusaini mkataba wa kurejea Atletico Madrid.

kwa mara nyingine tena akitokea Chelsea.Diego Costa tayari amepewa jezi namba 18 na Atletico Madrid hivyo tutaanza kumuona akiivaa rasmi mwezi January 1 atakapoanza kuichezea katika mechi za mashindano, Costa amesaini mkataba baada ya kufuzu vipimo vya afya alivyofanyiwa Jumamosi na Jumatatu.Hata hivyo Diego Costa atajiunga na timu na kuanza kufanya mazoezi lakini hatokuwa na nafasi ya kuichezea hadi dirisha la usajili la majira ya baridi la January litakapofunguliwa, kama utakuwa unakumbuka vizuri Costa alijiunga na Chelsea 2014 akitokea Atletico Madrid aliyodumu nayo kwa miaka minne.

story@moodyhamza