Messi afanya maajabu Barcelona

Lionel Messi alifunga mabao manne na kuwasiadia viongozi wa La Liga Barcelona kuendeleza rekodi yao ya kushinda mechi zote msimu huu kwa kuandikisha ushindi mkubwa dhidi ya Eibar.

Messi alifunga mkwaju wa penalti na kuwaweka wenyeji hao kifua mbele kabla ya Paulinho kufunga la pili kwa kichwa.

Denis Suarez kisha alifunga kutoka kwa mpira wa kudunda lakini Sergi Enrich akawakombolewa Eibar bao moja na kufanya mambo kuwa 3-1.

Messi alifunga mabao mawili katika muda wa dakika moja kabla ya kubadilishana pasi murua na Aleix Vidal na kufunga bao lake la nne dakika za mwisho kwenye mechi hiyo.

Ushindi huo unawaweka Barcelona uongozini wakiwa na alama 15, alama tano mbele ya Sevilla walio wa pili ingawa Barca wamecheza bao moja zaidi.

Messi kwa mara nyingine anaonekana kung’aa mbele ya wavu.

story@moodyhamza