Karim Benzema anafuraha Real Madrid licha ya tetesi za Arsenal

Karim Benzema anafurahia kuendelea kubaki Real Madrid na hana mpango wa kuihama klabu hiyo, kwa mujibu wa wakala wake

Habari kutoka Hispania Jumatano zilidai kuwa Arsenal imetoa ofa kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kuelekea dirisha la uhamisho Januari.

Benzema amsaini mkataba mpya wa miaka minne Real Septemba na mwakilishi wake, Karim Djaziri, amezifutilia mbali tetesi hizo za kuondoka kwa mchezaji huyo Bernabeu.

“Karim Benzema anafuraha sana Real Madrid,” Djaziri alikiambia Sky Sport News.

“Amesaini kuongeza mkataba mwezi uliopita na kwa hakika hana mpango wa kuondoka klabuni.”

Benzema alijiunga na Real 2009 na amefunga magoli 182 katika mechi 373 alizocheza, akiisaidia klabu kushinda mataji mawili ya La Liga na matatu Ligi ya Mabingwa Uefa.

Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger alivunja rekodi ya usajili ya klabu msimu wa majira ya joto kwa kumsajili Alexandre Lacazette kwa paundi milioni 53, na bado anao wachezaji wengine mahiri kama Alexis Sanchez, Theo Walcott, Olivier Giroud na Danny Welbeck.

@moodyhamza