Jeraha la nyuma ya goti la kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba’s limmuweka nje

Jeraha la nyuma ya goti la kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba’s limmuweka nje kwa kiindi kirefu , kulingana na mkufunzi Jose Mourinho.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliguchia na kutolewa nje dakika 19 za mechi ya vilabu bingwa kati ya The Reds na Fc Basel na tayari amekosa mechi nne zilizopita.

ilidhaniwa kuwa Pogba kwamba mchezaji huo atakuwa nje kwa kati ya mwezi moja na wiki sita kufuatia jeraha hilo mnamo tarehe 12 mwezi Septemba.

Mourinho hata hivyo hakuweza kutoa muda rasmi wa kurudi kwake.

Mourinho alisema kuwa hazungumzii kuhusu majareha ya muda mrefu lakini alikuwa na matumaini makubwa kuhusu beki Phil Jones na Antonio Valencia.

”Siwezi kuwa na matumaini, kama vile Jones ama Valencia ninapowaona katika mazoezi na natumai kutakuwa na jibu” ,aliongeza raia huyo wa Ureno.

Kiungo wa kati Michael Carrick na Marouane Fellaini pia anatarajiwa kukosa mechi ya Jumamosi nyumbani dhidi ya Crystal Palace.

story@moodyhamza