Kenya imepokonywa fursa ya kuandaa mashindano ya ubingwa wa Afrika wa mwaka 2018 (CHAN)

Hatua hiyo ilitangazwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari baada ya mkutano wa siku moja uliioongozwa na rais wa Caf Ahmad.

Caf inasema uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kuchelewa kwa ripoti za ukaguzi kadha uliofanywa nchini Kenya.

Kinyanganyiro hicho ambacho kitashirikisha timu 16 kinatarajiwa kuanza tarehe 12 Januari hadi Februari mwaka 2018.

Timu ya ukaguzi ya Caf ilizuru Kenya kuanzia tarehe 11 hadi 17 mwezi huu, na kupata kuwa ni uwanja mmoja tu kati ya viwanja vinne uliokuwa tayari kwa michuano hiyo.

Shirikisho la kandanda nchini Kenya (FKF) linasisitiza kuwa lilifanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa mashindano ya CHAN mwaka 2018 yangewezekana kwa Kenya na eneo lote la Afrika Mashariki.

story@moodyhamza