Meneja wa timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza Mark Sampson,atimuliwa

Meneja wa timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza Mark Sampson, ambaye amekuwa akitumiwa kwa ubaguzi wa rangi sambamba na matumizi ya nguvu amefukuzwa.

Chama cha soka cha Uingereza FA kimesema kufukuzwa kwake kunafuatia kuthibitishwa kwa tuhuma zilizokuwa zikimkabili ambazo awali zilikuwa zikifanyiwa upelelezi.

Awali mshambuliaji wa timu hiyo Eniola Aluko alimtuhumu Sampson kwa ubaguzi.

Sampson amekana tuhuma hizo na kusema ni hujuma juu yake.

story@moodyhamza