Majibu ya Barnaba kuhusu kuachana na Mama Steve

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa za kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi kati ya Barnaba na mama mtoto wake mama Steve ambapo Barnaba alikuwa akizikanusha akisema hawajatofautina.

March 22, 2017 Barnaba Classic ameweka wazi juu ya ishu hiyo kupitia XXL ya Clouds FM ambapo amesema ingawa walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mama Steve kwa miaka tisa, lakini sasa wamechana,

Barnaba amejibu swali ambalo aliulizwa na B Dozen aliyemuliza kama wameachana na mama Steve ambapo alijibu...>>>”Mimi na Mama Steve hatupo pamoja kwa sasa, tumedumu kwa miaka tisa’ Nam-respect sana mama Steve ila kila mtu anaendelea na maisha yake na hatutaki kutengeneza picha mbaya kwa mwanetu.

 “Sipendi kuzungumzia sana uhusiano wangu ila tumeachana muda mrefu na tupo vizuri tu hakuna shida. Wimbo wangu mpya sijamuimbia mtu na hauhusiani na maisha yangu kabisa” – Barnaba.

 

Source: Millard ayo