Diva afwata nyayo za kim kardashian

 

Mtangazaji wa kituo cha radio cha Clouds Fm, Diva The Bawse ameamua kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kufanya biashara kistaa zaidi.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni mrembo huyo ambaye amekuwa akipendwa na watu kutokana na uzuri wa sauti yake, amesema ameamua kuingia katika biashara kwani alikuwa na ndoto ya kufanya hivyo kwa muda mrefu.

“Nimeamua kufanya biashara ya vipodozi kwa njia ya mtandao, hii ni ndoto yangu ya muda mrefu sana nimevutiwa zaidi ufanya biashara hiyo kistaa zaidi kama wanavyofanya mastaa kutoka nje, unajua ukifanya biashra kwa njia hiyo unaingiza hela zaidi,” amesema Diva.

Source: Udaku