Msanii Chinbees Awekwa Chini Ya Ulinzi.


Mwanamuziki kutoka lebo ya ‘Wanene Entertainment’, Chin Bees anashikiliwa na Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam kwa kosa ambalo mpaka sasa halijawekwa wazi.

Hayo yamebainishwa na meneja wake Darsh asubuhi ya leo baada ya msanii wake kushindwa kuhudhuria kipindi ya FRIDAY NIGHT LIVE ‘FNL’ kutoka EATV usiku wa jana (Ijumaa).
“Naomba radhi kwa kitendo kilichotokea jana kwa msanii wangu Chin Bees kushindwa kuja katika ‘show’ kutokana na kushikiliwa na polisi baada ya kubainika kufanya kosa alipokuwa katika show yake huko Zanzibar ambako mpaka sasa haijawekwa wazi”, alisema Darsh.
Chin Bees kwa sasa anasubiriwa kupelekwa visiwani Zanzibar kwenda kujibu tuhuma zake ambazo zinamkabili.

Source: Udaku.