Christian Bella Aja Na Ngoma Mpya.


KING Of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ kwa mara ya kwanza baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu amefunguka kuwa anatarajia kuachia ngoma mpya Septemba 3, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem.  Christian Bella alisema kuwa usiku huo mashabiki wake wajitokeze kwa wingi kumsikia akipiga ngoma zake zote kali kuanzia Safari Siyo Kifo, Nashindwa, Ollah, Nishike, Nani Kama Mama na nyingine nyingi.

Kwa mara ya kwanza nitapiga nyimbo zangu zaidi ya 20 live kwa kutumia vyombo pia nitatambulisha ngoma yangu mpya kabisa,” alisema Bella. Naye Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema siku hiyo itatambulika kama Naja Dar Live ambayo mbali na uwepo wa Bella pia atakuwepo mkali wa Bongo Fleva anayekimbiza na Wimbo wa Ngoma Droo, Pamela Daffa ‘Pam D’.

“Pam D atawakosha mashabiki wake kwa nyimbo kali kuanzia Popolipopo, Nimempata, Daffa na huu wa sasa wa Ngoma Droo akiwa na Bella tena siku hiyo watauimba live kwa kutumia vyombo,” alisema Mbizo na kuongeza; “Mbali na Bella na Pam D, Dar Live itashuhudia kwa mara nyingine kundi kongwe la Muziki wa Pwani lisilo na mpinzani kwa sasa la Zanzibar Stars likihamishia mashambulizi Dar Live likiwa chini ya wakali kibao akiwemo Bi.Mwanahawa, Jokha Kassim, Mosi Suleiman, Ally Jay pamoja na Issa Kamongo, utakosaje sasa?”

Source: Udaku.