Msanii Ruby Akanusha Uvumi.

Ruby ametolea ufafanuzi tetesi za kuwa ni mjamzito.  Mrembo huyo amasema tatizo la watanzania wengi wanapenda kujipa majibu wenyewe ambayo kwa asilimia kubwa yanakuwa sio ya kweli.

“Maneno wameumbiwa binadamu na huwezi kuyazuia,” amesema. “Ila kiukweli kabisa leo hii nathubutu kusema kuwa mimi sina mimba na sijawahi kuwa na mimba isipokuwa ile nguo niliyokuwa nimevaa ilikuwa inaonesha hivyo na hiyo siku nilikuwa nimetoka kula na pozi pia ambalo nilikuwa nimeweka so ikapelekea kuonekana nina mimba lakini nakanusha mimi sina mimba,” amesisitiza.

Kwa siku za karibuni Ruby alikuwa amewaacha njia panda mashabiki wake baada ya kupost picha kwenye mtandao wa Instagram akionekana kama ni mjamzito.

Source: Dizzim Online.