Sauti ya Diamond akikiri kuwa na mtoto kabla ya Tiffah

  ya leo  inamuhusu Mwimbaji Diamond Platinumz kudaiwa kuwa na mtoto kabla ya Tiffah na Prince Nillan ambapo mtangazaji Soudy Brown kabla ya kuzungumza na kaka wa dada anayedaiwa kuzaa na Diamond aliicheza sauti anayosikika Diamond akikiri kuwa alikuwa na mwanamke Mwanza ambaye aliwahi kusema ana ujauzito wake na mpaka alikuwa akimhudumia

Kwenye sauti hiyo Diamond amesikika akisema ….>>>“Niliwahi kwenda mwanza zamani nilikuwa katika show ya matamasha makubwa nikakutana na mtoto kawaka alikuwa anatokea kwenye chumba cha Brother Dully, akaja kwangu Mimi nikafanya yangu” :-Diamond

“Nilivyorudi huku demu akanambia  ana mimba nikaanza kuhudumia, nikaenda mwanza kumtafuta japo kwao walini-Mind wakaona kama nazingua, nikambana kujua ukweli kama ana mtoto, maana alinidanganya kuwa katoa Mimba,

Nilipomchunguza nikajua kweli amezaa nikamuomba nimuone mwanangu hata kwenye picha ndipo asubuhi akaondoka pale hotelini tulipokuwa ili akaniletee picha nimuone,  alivyoondoka muda wa ndege yangu kuondoka ulikuwa umefika akawa amechelewa kurudi, nilivyompigia simu akakataa kunitumia picha kwa simu” :-Diamond

Soudy brown alipo mtafuta mama wa mtoto pamoja ndugu wa karibu hakufanikiwa zaidi ya kaka wa Dada anayesemekana kazaa na Diamond…..>>>“Ni kweli Diamond kazaa na dada yangu, ni mtoto wa mama yangu mdogo, anaitwa Anita anafanya kazi ya Salon na mtoto huyo anafanana na Diamond kila kitu na mtoto ana miaka mitano au sita na mtoto anaitwa Queen yaani ukimuangalia mdomo ule ule japo mama yake kaolewa” …….. by milard ayo………..