Taarifa feki inayodaiwa kutoka Ikulu Dar es Salaam

Saa kadhaa baada ya Rais John Pombe Magufuli kumuapisha Waziri mpya wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba, kumekuwa na taarifa inayoenea mitandaoni ikieleza kuwa imetoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Taarifa hiyo ambayo ilikanushwa kupitia ukurasa rasmi wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa, inaeleza kuwa serikali imesema itafungia matumizi ya mitandao ya kijamii endapo itabaini hayana tija yoyote nchini.

Hii ndio taarifa feki inayosambazwa na kudaiwa kuwa imetoka Ikulu Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu

Source: Millard ayo