Chelsea kifua mbele ugenini mechi ya vilabu bingwa ya kundi C.

Michy Batshuayi alifunga dakika za lala salama na kuisaidia Chelsea kupata ushindi mwembamba dhidi ya Atletico Madrid na hivyobasi kuendeleza rekodi ya kutofungwa katika mechi ya vilabu bingwa ya kundi C.

Batshuayi aliugusa mpira akiwa katika eneo hatari na hivyobasi kupata bao katika dakika ya 94 kutoka kwa krosi iliopigwa na Marcos Alonso.

Chelsea ilikuwa nyuma kunako dakika ya 40 baada ya penalti licha ya kutawala kipindi cha kwanza wakati David Louis alipomvuta shati Lucas Hernandez wakati wa kona.

Lakini Chelsea , ambao waligonga mwamba kupitia Eden Hazard katika kipindi cha kwanza walionyesha mchezo mzuri wakati wa kipindi cha pili na wakasawazisha kupitia Alvaro Morata.

Mchezaji huyo wa Uhispania alifunga kwa kutumia kisigino baada ya kupata krossi murua.

Bao la ushindi la Batshuayi’s lilijiri baada ya Cesc Fabregas na Morata kukosa nafasi za wazi huku Chelsea ikiwa timu ya kwanza ya Uingereza kushinda katika uwanja wa Atletico huku timu hiyo ikisema kuwa kushindwa kwao kunatokana na uwanja mpya waliopata.

story@moodyhamza