Ronaldo kufikisha jumla ya game 400 akiichezea Real Madrid

Usiku wa September 26 2017 michezo nane ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018 ilichezwa barani Ulaya, moja kati ya mchezo wa kuvutia ulikuwa ni mchezo kati ya Borussia Dortmund dhidi ya Real Madrid ya Hispania ambao walikuwa ugenini.Real Madrid leo wakiwa ugenini wamefanikiwa kupata ushindi wa pili wa Champions League wa magoli 3-1 dhidi ya wenyeji wao Borussia Dortmund ya Ujerumani, magoli ya Real Madrid yalifungwa na Gareth Bale dakika ya 18 na Cristiano Ronaldo aliyefunga magoli mawili dakika ya 50 na dakika ya 79.Kufunga magoli mawili kwa Ronaldo kunamfanya kuzifunga timu za Ujerumani kwa mara ya 25 akicheza dhidi yao kwa mechi 21, hata hivyo usiku huo umemfanya Ronaldo kufikisha jumla ya game 400 akiichezea Real Madrid akiwa kafunga jumla ya magoli 411, assist 111 na amefunga jumla ya hat-trick ya 42.

story@moodyhamza