Bingwa wa ndondi uzito wa kati duniani Andre Ward amestaafu

Bingwa wa ndondi uzito wa kati duniani Andre Ward amestaafu mchezo huo ikiwa ni mapema tofauti na ilivyotarajiwa.

Ward mwenye miaka 33 ameshinda mataji matatu tofauti ya uzani wa kati ikiwa ni pamoja na WBA, IBF na WBO.

Katika taarifa yake amesema mwili wake haupo tiyari kupata magonjwa ya kutetemeka.

”Kama siwezi kuipa familia yangu,timu yangu na mashabiki yangu kile wanachokitaka, basi sipaswi kuendelea kupigana,”alisema.

Mapema wiki hii Ward alituma picha kwenye mitandao ya kijamii akionyesha baadhi ya mikanda yake aliyoinyakua siku za nyuma.

Mara ya mwisho alipigana mwezi June na kumtangwa Sergey Kovalev mjini Las Vegas.

story@moodyhamza