Paris St-Germain iliinyamazisha miamba ya Bayern katika mechi ya mabingwa

Paris St-Germain iliinyamazisha miamba ya Bayern katika mechi ya mabingwa ili kupanda juu kwa pointi 3 katika kilele cha kundi B.

Dani Alves aliwafungia wenyeji bao la kwanza baada ya sekunde 84 kufuatia pasi nzuri ya Neymar.

Alphonse Areola aliokoa shambulio kali na kumyima bao Javi Martinez kabla ya PSG kuchukua alama zote tatu.

Shambulizi la kwanza la Edinson Cavani lilifanya mambo kuwa 2-0 kabla ya Neymar kufunga bao la tatu.

Mara ya kwanza kwa PSG kucheza dhidi ya klabu kubwa ya Ulaya katika kombe la vilabu bingwa walicharazwa 6-1 na Barcelona katika awamu ya mwisho ya mechi za makundi msimu uliopita.

story@moodyhamza