Msemaji wa Simba SC Haji Manara

Msemaji wa Simba SC Haji Manara jana September 27, 2017 amekutana na Waandishi wa Habari Mwanza na miongoni mwa aliyozungumzia ni kuhusu Kocha wa Klabu hiyo Joseph Omog baada ya baadhi ya mashabiki kuonesha kutoakuwa na imani naye.

“Hatuiwezi kuachana na kocha Omog, naomba hilo mliondoe kabisa akilini mwenu, suala la matokeo linategemeana na mchezo wenyewe, kocha lazima aangalie kikosi alicho nacho ndipo anapanga wacghezaji, wala hakuna kiongozi ambaye anaweza kumuingilia kocha kupanga kikosi.

“Hata kama ungekuwa na kikosi kizuri namna gani, hakuna timu ambayo kila mechi lazima itashinda, suala la mashabiki kulaumu ni la kawaida. Omog ameangalia mashabiki wana kiu ya ubingwa hivyo anatumia mfumio ambao utampa matokeo kulingana na wachezaji waliopo,” alisema Manara.

Aidha Manara amesisitiza kuwa klabu yake haitamuondoa Omog kwani anafanya vizuri na wana uhakika wataibuka washindi kwenye mashindano yote yaliyoko mbele yao.

story@moodyhamza