Staili 3 za Kujamiana Ambazo ni Hatari.

Tafiti zimebaini kuwa hizi ndizo aina kuu tatu za ufanyaji wa mapenzi zinazoweza kupelekea mwanaume kupata madhara ya kuvunjika kwa uume.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika ‘dog style’, ‘missionary’ na ‘cowgirl’ zimeelezwa kuwa ndizo zinazoongoza zaidi kusababisha kuvunjika kwa uume.

Ripoti iliyochapishwa katika jarida la “international journal of Impotence” ilichunguza wanaume 90 wenye umri wa kati ya miaka 18-66 walikumbwa na tatizo la kuvunjika kwa uume.

Utafiti huu uliwagawanya waathirika hao katika makundi sita kulingana na ukubwa wa tatizo ambayo yalihusisha: Punyeto, aina ya ufanyaji wa mapenzi ambao mwanaume huwa juu ‘missionary’, ‘dog style’, ufanyaji wa mapenzi ambao mwanamke hukaa juu ‘Cowgirl’ na nyinginezo.

Utafiti ulibaini kuwa wanaume 69 kati ya wenye madhara ya kuvunjika kwa uume wamesababishwa na ufanyaji wa mapenzi.
Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa wanaume 37 walipata madhara ya kuvunjika kwa uume kutokana na kufanya mapenzi kwa aina ya ‘dogstyle’

Wanaume 23 walipata madhara ya kuvunjika kwa uume kutokana na ufanyaji wa mapenzi wa aina ambayo mwanaume hukaa juu wengi huiita ‘kifo cha mende’ au ‘missionary style’.

Aina ya ‘dogstyle’ iliripotiwa kusababisha madhara kwa wanaume wengi kuliko aina nyingine japo madhara yake hayakutofautiana sana.

Unashauriwa kutambua ni aina ipi ya ufanyaji wa mapenzi ambayo inaweza kukusababishia madhara ya kuvunjika kwa uume na kama unaipendelea basi ni vyema ukaifanya kwa uangalifu mkubwa, japokuwa wakati mwingine inakuwa ni vigumu kukumbuka.

Source: Udaku.