Mama kamtelekeza mwanaye wa miezi 7.

Hekaheka ya Leo Tena ya Clouds FM leo September 27, 2017 , inamuhusu dada aliyemkimbia mumewe na mtoto wake mwenye miezi 7 na kudai kuwa maisha ya ndoa yamemchosha.

Ni baada tu ya kumtelekeza mtoto wake kwenye nyumba ya jirani, na kudai kuwa amechoshwa na maisha ya ndoa na kutaka kujitafutia maisha yake mwenyewe, na mama yake kudai kuwa mtoto huyo bado anahitaji kunyonya kwani bado ni mdogo sana, na kumtaka binti huyo arudi nyumbani ili aendelee kumtunza mwanaye.

Source: Millard ayo.