Leo ndio ile siku ambayo wapenda burudani wa mkoa wa Dodoma walikuwa wanaisubiri kwa hamu kubwa kwa mwaka huu kuotkana na kuwa na kiu ya burudani iliyodumu kwa zaidi ya miezi 23 hadi sasa.
Mida flani hivi ya jioni itaandikwa historia katika uwanja wa Jamuhuri Stadium kwa kudondoshwa bonge moja la show kutoka kwa wasanii wakali na wanaofanya vizuri kwenye soko la muziki kwa sasa.
Kabla ya tukio hilo la kihistoria hapo jioni, asubuhi ya leo timu nzima ya Fiesta wakiwemo na wasanii walihudhuria kikao cha 8 cha mkutano wa 4 wa Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mjini hapo na kamati ya Fiesta kuweza kukabidhi kiasi cha Shilingi za kitanzania Million 40 kama mchango kwa wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililo itikisa kanda ya ziwa siku chache zilizopita.
Tazama hapa kwa picha jinsi ilivyokuwa Bungeni hapo asubuhi ya leo.
Story By:@Joplus_
Source: Perfect255.com