STAA TAYLOR SWIFT AMBWAGA MPENZI WAKE TOM HIDDLESTON.

Baada ya miezi mitatu tu kwenye mahusiano pop staa Taylor Swift ameachana na mpenzi wake Tom Hiddleston.

Sababu ya wawili hawa kuachana imetajwa kuwa ni kauli ya Taylor kuwa hakutaka mahusiano yake ya Tom kuwa wazi sana sababu sio kitu anachotaka kwa sasa.

Taylor Swift alihamia nyumba moja na staa huyu Muingereza muda mfupi tu baada ya kuanzisha mahusiano yao ikiwa ni wiki mbili tu baada ya kuachana na boyfriend wake Calvin Harris  June mwaka huu.

Story By:@Joplus_

Source: Sam Misago.