Sahau kuhusu Bongo Fleva – sasa ulingo umevamiwa na wasanii wa Singeli. Mfalme wa muziki wa Singeli, Sholo Mwamba amefunguka baada ya mfalme mwenzie, Man Fongo kumtuhumu msanii huyo kuwa ndiye aliyesababisha kutoelewana kati yake na Wema Sepetu baada ya kufikisha taarifa za umbea.Muimbaji huyo amesema kuwa Man Fongo anatafuta kiki kwakuwa amezoea kuropoka.“Mdogo wangu anatafuta kiki, huu ni muziki anatakiwa afanye kazi mambo mengine yaendelee. Yule alikuwa Dj wangu [Man Fongo] kwahiyo sina matatizo naye.”“Sitaki kumtafuta kwa sababu anaweza kuzusha kuwa nimempigia simu nimemuomba collabo,” ameongeza.
Msanii huyo amedai kuwa yeye hakumpigia simu mama Wema wala hiyo namba yake ya simu hajawahi kuwa nayo na amewahi kuonana naye mara moja tu.
Story by:@Joplus_
Source:Raha za walimwengu.