Baada ya Byser kutangaza kuchukua hatua za kisheria kwa Naj au Baraka endapo atagundua kuwa wao ndiyo walianzisha ile skendo iliyomuhusisha yeye kuwa anachepuka na Naj ili kuupa ‘kiki’ wimbo wao mpya, eNewz ilimtafuta Naj ili kusikia majibu yake.Naj alisema “Sioni kama kuna tatizo, ila naona tu haya mambo yanakuzwa na maneno ya watu, Mimi huwa sifanyi kazi kwa ‘kiki’, na kwa sasa chochote nitakachokisema ninaweza nisieleweke hivyo nimeamua ni bora nikae kimya tu”.Pia Mr. Blue a.k.a Byser alisema kuwa aliongea na Baraka na Baraka akasemea kuwa hajui uzushi huo umetokea wapi, hivyo wakayamaliza bila ya kuwa na tatizo.
Hata hivyo Byser alimaliza kwa mkwara akisema “Kama hawa watoto wadogo ni wao ndiyo wameanzisha hii skendo, nikigundua ni hivyo basi nitawachukulia hatua, na pia mimi siwezi kurudia matapishi yangu”.
This website uses cookies to improve your experience while you navigate through the website. Out of these cookies, the cookies that are categorized as necessary are stored on your browser as they are as essential for the working of basic functionalities of the website. We also use third-party cookies that help us analyze and understand how you use this website. These cookies will be stored in your browser only with your consent. You also have the option to opt-out of these cookies. But opting out of some of these cookies may have an effect on your browsing experience.
Necessary cookies are absolutely essential for the website to function properly. This category only includes cookies that ensures basic functionalities and security features of the website. These cookies do not store any personal information.