GIGY MONEY AFUMWA AKICHEPUKA.

Baada ya kurukaruka na wanaume tofauti, hatimaye msanii na Video Queen Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’, amejikuta akichezea kichapobaada ya kufumaniwa akiwa na mchumba wa mtangazaji wa Choice FM aliyetajwa kwa jina moja la Mo, nyumbani kwake Kawe jijini Dar.

Video Queen Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money akiwa katika mapozi tofauti.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Gigy amekuwa hatupii picha za aina yoyote kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa sababu ya majeraha aliyopata baada ya msichana aliyefahamika kwa jina la Shov Mohamed kumfumania nyumbani hapo kwa Gigy.
“Mnajua Gigy hivi karibuni alifumaniwa nyumbani kwake na mwanaume wa mtu akapata kipondo hevi mpaka hivi ninavyowaambia majeraha ndiyo kwanza yanaanza kupoa na mara nyingi amekuwa akificha majeraha ya usoni kwa kujipaka make up kwa wingi kama akitaka kutoka.
“Shov alimfumania baada ya kwenda kwa Mo anayeishi jirani na Gigy, akagonga mlango bila kuitikiwa ndipo alikuja mtu akamtonya kuwa amemuona Mo anaingia nyumbani kwa Gigy ndipo akaamua kumfuata.
“Alipofika ndani alikuta mambo ambayo moja kwa moja yaliashiria kuwa mwanaume huyo na Gigy ni wapenzi ndiyo pakaanza kuchimbika. Unaambiwa Gigy alizidiwa nguvu na kupewa kipondo na Shov kisha mwanaume akachomoka eneo hilo na kumuacha Gigy povu la matusi likimtoka,” alisema Sosi.
Baada ya wanahabari wetu kunyaka ubuyu huo walimtafuta Gigy, alipapotikana alikiri kufumaniwa: “Ni kweli nilifumaniwa na ninamwambia huyo mwanamke ajipange kwani kwa Mo ndiyo kwanza nimefika, sitegemei kumuacha leo wala kesho, kifupi umalaya siachi si k w a kufumaniwa ndiyo kwanza nimeanza moja.
“Unajua wakati naanza uhusiano na Mo sikujua kama ana mwanamke na sasa uhusiano umeshakuwa na nimemzoea ndiyo nagundua unadhani nitamuachaje, yeye akae asubiri ndiyo kwanza kumekucha nitampa mapenzi mpaka atamsahau hata huyo mwanamke wake,” alisema Gigy.
Mbali na Mo, Gigy ametajwa kubanjuka penzini na mastaa wengi akiwemo Mtangazaji Gardner G. Habash ‘Captain’, Hemed Suleiman, Omar Faraj Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, Idris Sultan, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ na Abdul Kiba.

Story by:@Joplus_
Source:Raha za walimwengu.