DIVA THE BAWSE AFUNGUKA KUHUSU PICHA ZAKE ALIZOPOST KUPITIA INSTAGRAM YAKE.

Mtangazaji maarufu wa vipindi vya usiku anaesimamia show ya Ala za Roho inayoruka Clouds Fm kila Jumatatu – Alhamis saa 4-6 usiku Diva The Bawse amekuwa akimake headlines katika mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akipost picha katika ukurasa wake wa Instagram zinazomuonyesha akiwa kavaa nguo za ndani.

BK-ANF8gNZE
Diva The Bawse kwenye ubora wake

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Instagram na umem-follow mwanadada huyo naamini utakuwa umekutana na picha hizo.

Soudy Brown ameamua kumvutia waya (Kumpigia simu) mwanadada huyo na kumuuliza ni kipi kinaendelea kwasababu mrembo huyo hakuwa na tabia hiyo hapo awali.

Diva amedai kuwa hayo ndio maisha yake na wala hatojali kupoteza mashabiki kwa kitendo chake hicho kwasababu kama wameamua kumpenda inabidi wampende kama alivyo.

Yapo mengi ambayo ameyazungumza mwanadada huyo, interview nzima nimekuwekea hapa chini kwenye hii video. Itazame.

Story by:@Joplus_

Source: Perfect255.com