JUMA NATURE: T.I.D NDIYO CHANZO CHA KR KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA.

Wiki iliyopita tulizinyaka headlines za mkongwe wa muziki wa bongo fleva K.R kukutwa amezima kabisa barabarani Mbagala Rangi Tatu kwa kilichosemekana kuwa ni pombe.Tokeo la picha la jUMA NATURE NA k.r

Mengi yaliongelewa na wengi walisikika juu ya suala hilo ikiwemo aliiyekuwa kiongozi wa kundi la Wanaume TMK Family Juma Kassim Nature na kuonekana kusikitishwa sana na kitendo hicho.

Juma Nature alipiga story na E-News ya EATV na kudai kuwa T.I.D ndio chanzo cha yote hayo.

Juma Nature alisema kuwa yeye alitumiwa picha na wadau, na hakuona sababu ya kuacha kumsaidia kwasababu yule ni ndugu yake na wametoka mbali japokuwa alishawahi kumzungumzia vibaya lakini yeye hakujali hilo. Ndipo akachukua uamuzi wa kutuma gari kwenda kumchukua na kumfikisha nyumbani kwake Juma Nature.

Juma Nature alifunguka kuwa yeye alikuwa amekwisha lifahama hilo hapo awali tangu tu aliposikia K.R anataka kujiunga na kina T.I.D na akajua kuwa lazima watamuingiza kwenye utumiaji wa SEMBE.

Akiongea kwa msisitizo alidai kwamba ile iliyomfanya vile K.R ni SEMBE kwasababu pombe ya kawaida haiwezi kumfanya mtu vile.

K.R alitafutwa kwa muda wake na kuulizwa juu ya anachokiongea Juma Nature na alidai kuwa Nature analalama kwasababu hajui kinachoendelea. Alidai kuwa kelele za Nature wala hazimpi tabu. “Acha aendelee kulalama huku mi nafanya yakwangu,”
Ni kauli iliyotoka mdomoni mwa K.R

K.R aliongeza kuwa kinachomuumiza ni kitendo cha Juma Nature kumpakazia kwenye vyombo vya habari kwamba yeye anatumia SEMBE wakati kitu hicho sio cha kweli.

Huku Nature nae akiendelea kusisitiza kuwa K.R ni mshkaji wake na wala hana tatizo nae, endapo atajisikia kurudi TMK yeye awe huru tu wala hana tatizo nae.


KAMA ULIPITWA NA U-HEARD YA K.R ALIYOKUTWA AMELALA MTALONI ITAZAME HAPA UYASIKIE MAPOVU YA JUMA NATURE.

Story By:@Joplus_

Source:Perfect255.com