JOKATE: MUZIKI BADO NAFANYA ILA BADO NAHITAJI MANAGEMENT AMBAYO ITANISIMAMIA VIZURI.

Mwanamitindo na mwanamuziki nchini Tanzania, Jokate Mwegelo ambaye amekuwa kimya katika masuala ya muziki kutokana na kuwa busy na biashara, amesema bado anafanya muziki.

Jokate ambaye wimbo wake wa mwisho kuutoa ulikuwa ‘Leo Leo’ aliomshirikisha Ice Prince kutoka Nigeria, alikuwa akihojiwa Ijumaa hii kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

“Muziki bado nafanya ila bado nahitaji menejimenti ambayo ipo vizuri,” alisema. “Sitaki kufanya muziki niwe kama najaribu, nahitaji kuwa na timu ambayo tutafanya kazi ya serious kama ilivyo kwenye brand ya Kidoti. Bado natafuta timu ambayo itanisimamia katika muziki vizuri, sijaacha nimesimama tu hadi hapo nikapopata menejimenti nzuri,” alisema Jokate.

Story By:@Joplus_

Source: Udaku Special Blog