RAPPER WITNESS AMEFUNGUKA NA KUSEMA ALIAMUA KUCHORA TATTOO YA JINA LA MPENZI WAKE ILI ASICHEPUKE.

Mwanamuziki wa muziki wa kufoka foka nchini Tanzania, Witness, a.k.a Witness kibonge Mwepesi, ameelezea sababu ya kuchora tattoo yenye jina la mpenzi wake wa sasa Ochu Sheggy katika kiuno chake.

Akizungumza ndani ya eNewz amesema “Ukiweka tattoo sehemu niliyoweka mimi inazuia hata unapotaka kumsaliti mwenza wako yule unayekuwa naye ina kunyima hamu kabisa na anashindwa hata kukutamani tena”.

Pia aliendelea kusema kuwa watu wanadhani kuwa kuolewa ndiyo kumaliza kila kitu lakini kwa sehemu ambayo mapenzi yao yamefikia hakuna kitu ambacho anakihitaji tena kwa kuwa mapenzi ni kuungana mkono na Ochu anamsaidia katika kila kitu ninachofanya.

Story By: @joplus_
Source: Udaku Special Blog.