Kiungo wa kati wa Barcelona Ivan Rakitic amesisitiza kuwa sio rahisi kucheza na Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez vile watu wanavyodhania.
Washambuliaji hao waliisaidia Barcelona kushinda mataji matatu ya ligi pamoja na yale ya klabu bingwa Ulaya na wamepongezwa kuwa washambuliaji mahari zaidi duniani.
Rakitic anasema kuwa wachezaji wengine wanafurahia kuwahudumia washambuliaji hao, lakini akakiri kwamba ni vigumo kuwazuia wanaposhirikiana.
”Watu wengi husema kuwa ni rahisi kucheza nao”, alisema. ”Sikubaliani nao. Ni Wachezaji wa kiwango tofauti na tunapocheza nao ni kwa kuwa ni haki yao lakini haimaanishi kwamba ni rahisi. Na iwapo utahitajika kukimbia kilomita 5,000 ili mmoja wao kuweza kucheza vyema, nitafanya. Tunawafanyia”.
”Timu zote zingependa kucheza na Leonel Messi, lakini tunashukuru kuwa naye na tutamuhudumia kwa hali na mali”.
”Yeye hufanya vitu ambavyo hakuna mtu mwengine anaweza kufanya. Maisha ni rahisi ukicheza na yeye na iwapo unaweza kufanya mambo kuimarika zaidi basi ni bora zaidi”’.
Rakitic pia alisema kwamba anatarajia kuisaidia Bareclona kushinda mataji matatu zaidi kati ya sasa na mwisho wa mwaka huu.
Aliongezea: Kwa muda mfupi tutashiriki katika kuwania mataji mawili zaidi.
Kombe la Uefa Supercup na lile la Supercup ya Uhispania na mwishoni mwa mwaka kombe la dunia.
story@moodyhamza