Lengo la kuletwa Mitume wa Allah (s.w)

1. Adam (a.s)
2. Idrisa ( Enock) (a.s)
3. Nuhu (Noah) (a.s)
4. Hud (Heber) (a.s)
5. Salih (Metheusaleh) (a.s)
6. Ibrahim (Abrahim) (a.s)
7. Lut (Lot) (a.s)
8. Ismail (Ismael) (a.s)
9. Is-haq (Isaac) (a.s)
10. Yaaqub (Jacob) (a.s)
11. Yusuf (Joseph) (a.s)
12. Shu’aib (Jethro) (a.s)
13. Ayyub (Job) (a.s)
14. Mussa (Moses) (a.s)
15. Harun (Aaron) (a.s)
16. Dhul kifl (Ezekiel) (a.s)
17. Daud ( David) (a.s)
18. Sulayman (Solomon) (a.s)
19. Ilyaas (Elias) (a.s)
20. Al – Yassa’ (Elisha) (a.s)
21. Yunus (Johah) (a.s)
22. Zakariya (Zechariah) (a.s)
23. Yahya (John the Baptist) (a.s)
24. Isa (Jesus) (a.s)
25. Muhammad (s.a.w)

Lengo la kuletwa Mitume wa Allah (s.w)

Mitume wameletwa kuwa Waalimu na viongozi wa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuusimamisha Uislamu katika jamii kinadharia na kimatendo kama tunavyojifunza katika Qur-an: “Kwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukaviteremsha vitabu na Uadilifu (mizani) pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu. (57:25) “Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na kwa dini ya haki ili kuifanya ishinde dini zote, ijapokuwa washirikina watachukia.” (9:33, 61:9)

Mwisho wa Utume

Maswali ambayo huweza kuulizwa ni: Kwa nini wahyi ukatike? Kwa nini Mitume wasiendelee kuletwa hadi kiyama? Kwa nini Muhammad (s.a.w) afunge mlango wa Utume? Ili kulielewa vizuri suala hili la mwisho wa Utume yafaa kwanza tuzingatie kuwa kilicho muhimu na cha msingi kabisa kwa Mtume yeyote si kule kuwepo kimwili bali ni kule kuufikisha kwake ujumbe aliopewa na Mwenyezi Mungu (s.w) ili watu wake wasiwe na hoja tena iwapo watachagua kupotea. Na lau ingekuwa lililo muhimu kwa Mtume ni kule kuwapo kimwili basi Mwenyezi Mungu angelimpeleka Mtume mara tu baada ya kufariki Mtume aliyetangulia.

story@moodyhamza