Msanii wa Hiphop anayefanya vizuri sana kwasasa na ngoma yaje ya “Too Much” Darassa CMG amewatumia salamu za rambirambi wapenda Burudani wa Dodoma weekend hii kwenye msimu wa Fiesta.
Ni baada ya kudondosha shoo kadhaa za kibabe na hasa ile ya Kahama ambayo alipanda jukwaani na Mr Blue na hivyo kuahidi kuwa show kama zile huwa hazifanywi kila mara bali huwa inatokea tu kwa sehemu maalum.
“Tume fanya ile show na Mr Blue kahama lakini tunataka next time iwe kubwa zaidi ya ile. Watu wa Kahama wanaelewa kuwa ile show ndio ilikomesha kushinda zote na ndio sababu hatuwezi kufanya kila sehemu kwasababu tunahitaji maandalizi ya kutosha na show iwe kubwa pia.” Alisema Darassa.
Darassa aliongeza kwa kufunguka kuwa wakazi wa Dodoma wakae mkao wa kula kwa kudondoshewa bonge moja la show zaidi ya lile la Kahama. msikilize hapa
Story by:@Joplus_
Source:Perfect255.com