COLABO YA DRAKE NA WIZKID “ONE DANCE” YAWEKA REKODI YA SINGLE BORA INAYOONGOZA KWA MAUZO 2016.

Kismart cha star wa single ya Baba Nla , Ayodeji Ibrahim Balogun a.k.a Wizkid ambaye alipata nafasi kuperform kupitia Fiesta ya kwanza Jijini mwanza, kinazidi kuiweka Afrika kwenye ramani nzuri ya muziki kwa mara nyingine.

wizkidayo-20160919-0001

Wizkid anaingia kwenye headlines za kimataifa baada ya single aliyoshirikishwa na rapa kutoka YMCMB Drake ya One Dance kuongoza katika list ya nyimbo zinazouzwa zaidi duniani kwa mwaka 2016 huku ikiishusha single ya Justin Bieber iliyokua ikiongoza kipindi cha nyuma.

One Dance imetajwa kama “World’s best selling Single of 2016! Single ya Justin Bieber, Love Yourself’ iliweka rekodi hiyo mpaka kufikia mwezi August 2016.

Sasa mpaka kufikia mwanzoni mwa mwezi September 2016, One Dance ya Drake
na Wizkid inaongoza kwenye list hiyo.

‘Love Yourself’ imeshuka mpaka No.2 huku mzigo wa ‘Can’t Stop This Feeling’ wa Justin Timberlake ikiwa No.3. na ‘Stressed Out’ ya twenty one pilots ikishika No.4!

Story By:@Joplus_

Source:Perfect255.com